Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima iwepo mikakati ya sheria kupambana na ugaidi:Migiro

Lazima iwepo mikakati ya sheria kupambana na ugaidi:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amesema mataifa yote duniani lazima yawe na fumo wa kisheria na mikakati ya kupambana na ugaidi.

Amesema baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha maazimio kadhaa yaliyo na mtazamo wa kuzuia na kukabiliana na tishio hilo la kimataifa.

Akizungumza hii leo katika semina maalumu yenye mada kuwafikisha magaidi kwenye mkono wa sheria Bi Migiro amesema mikakati ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidui iliyopitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2006 inasisitiza mshikamano wa kulaani ugaidi wa aiana zote unaoofanywa na yeyote, popote na kwa sababu zozote zile.

Mkakati huo pia unahusisha elimu, maendeleo, kuzuia vita na mahusiano ya kimataifa. Migiro amesema sasa serikali zote lazima ziwe msitari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi kwa kuwa na mikakati imara ya kisheria.

(SAUTI YA ASHA MIGIRO)