Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza

WHO kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Shirika la afya duniani WHO linaongoza kampeni ya kimataifa ya kuwafanya viongozi wa dunia kuchukua hatua katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs.

Kwa mujibu wa WHO magonjwa hayo yakiwemo saratani, kisukari, magonjwa ya moyo na kiarusi yanahusika na zaidi ya asilimia 60 ya vifo vyote duniani.

Kwa kutambua umuhimu wa kudhibiti na kuzuia magonjwa hayo viongozi wa dunia wanatarajiwa kukutana Septemba mwakani mjini New York wakati wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuzungumzia magonjwa hayo. DR Alawan kutoka WHO anasema kukabiliana na mardhi hayo ni gharama kubwa.

(SAUTI YA DR ALAWAN)