Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuadhimisha siku ya ukimwi duniani UNICEF yazindua ripoti ya AIDS na watoto

Kuadhimisha siku ya ukimwi duniani UNICEF yazindua ripoti ya AIDS na watoto

Tarehe mosi Desemba kila mwaka huadhimishwa siku ya ukimwi duniani huku shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS, shirika la afya duniani WHO, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ,mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na wadau wa kupambana na ukimwi hutoa tathimini ya hatua zilizopigwa wapi palipo na mapungufu na nini kifanyike kuendelea kunusuru maisha ya watu kutokana na ugonjwa huo hatari usio na tiba hadi sasa.

Mwaka huu UNICEF na washirika wake wanatoa ripoti kuhusu ukimwi na watoto 2010 ambayo inatathimini hatua zilizopigwa katika maeneo manne ya HIV na ukimwi yanayoathiri watoto na kuelezea hatua muhimu za kuchukuliwa ili kufikia lengo la kuwa na kizazi kisicho na ukimwi.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa kwa ushirikiano wa UNICEF na washirika wake UNAIDS, UNESCO, UNFPA na WHO kikubwa walichobaini ni kwamba nchi nyingi zimepiga hatua katika kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa motto na katika matibabu ya kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa ripiti hiyo baadhi ya nchi zimepiga hatua katika lengo la kuzuia HIV na watoto wengi walioathirika na ukimwi wanfaidika na kulindwa, kupata huduma na msaada , lakini hata hivyo imesema bado juhudi kubwa zinahitaji kufanywa ili kutokomeza kabisa maambukizi mapya ya ugonjwa huo.