Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Asia ya Kati washiriki kusaka amani:Ban

Wanawake Asia ya Kati washiriki kusaka amani:Ban

Wanawake wa Asia ya Kati wametakiwa kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuleta amani kwenye kanda yao.

Akizungumza na wanawake mjini Astana makao makuu ya Khazakhstan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wanawake lazima wachangie katika kupambana na itikadi kali, usafirishaji haramu wa watu, na ukatili dhidi ya wanawake.

Ban amewaambia wanawake hao kwamba wanahitaji kushiriki mijadala na juhudi za kuzuia vita na migogoro. Amesema tunahitaji kujenga amani, lazima mshiriki sio tuu kama watazamaji, bali pia kama wafanya maamuzi, sio tuu kama waathirika ila kama mawakala wa kuleta mabadiliko.

Ameongeza kuwa kama mlivyo nyinyi nami pia ninahofia uwezekano wa kuongezeka kwa siasa kali, usafirishaji haramu wa watu na ukatili dhidi ya wanawake katika baadhi ya maeneo ya Asia ya kati.