Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa kisiasa kikwazo cha kupambana na kipindupindu Haiti

Mzozo wa kisiasa kikwazo cha kupambana na kipindupindu Haiti

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kupatikana kwa suluhu la haraka kwa mzozo wa kisiasa nchini Haiti baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi ulioandaliwa siku ya Jumapili akionya kuwa kuendelea kuwepo kwa ukosefu wa usalama huenda kukahujumu jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini humo.

Kwenye ujumbe wake Ban amesema kuwa anatafuta suluhisho la mzozo wa kisiasa uliopo nchini Haiti na kutoa wito kwa wananchi wa Haiti na wanasiasa kuwa watulivu akisema kuwa kuzorota kwa hali ya usalama kutakuwa na athari kwenye jitihada za kupamaban ana ugonjwa wa kipindupindu nchini humo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa idadi ya wanaoambukizwa ugonjwa wa kipindupindu inazidi kupanda sawia na wanaokufa kutokana na ugonjwa huo ambapo eneo la kaskazini mwa nchi ndilo lililoathirika zaidi.