Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu milioni 3 wataka serikali kukabili njaa:FAO

Zaidi ya watu milioni 3 wataka serikali kukabili njaa:FAO

Zaidi ya sahihi milioni tatu za watu wanaotoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kumaliza njaa duniani zimewasilishwa kwa serikali wakati wa sherehe zilizoandaliwa kwenye makao makuu ya shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO mjini Rome.

Ombi hilo linatoa wito kwa viongozi duniani kupambana na njaa. Makadirio ya shirika la FAO yanaonyesha kuwa watu milioni 925 wanakabiliwa na njaa kote duniani.

Pia mwaka uliopita hali mbaya ya uchumi duniani ilichangia idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa kupita watu bilioni moja kwa mara ya kwanza kwenye historia. Mkurugenzi wa shirika la FAO Jacques Diouf anasema kuwa watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanataka mabadiliko na kuwasihi viongozi wa kisiasa kuchukua hatua na kutatua tatizo la njaa.