Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama laongeza muda wa vikwazo DR Congo

Baraza la usalama laongeza muda wa vikwazo DR Congo

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha vikwazo vyake kwa baadhi ya raia ambao wanahusika na usafirishaji wa silaha haramu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wahusika wakuu wa vikwazo hivyo ni makundi ya waasi katika eneo la Kaskazini ambao wataendelea kupigwa marafuku kusafiri nje ya nchi pamoja na kusitishiwa kwa akaunti zao za nje.

Makundi hayo pamoja na kuendesha vitendo vya kihalifu, lakini pia yanatuhumiwa kwa kupora utajiri wa eneo hilo na kujinufaisha kwa maslahi binafsi.Pia yamekuwa yakihusika na ununuzi wa silaha haramu.