Viongozi pembe ya Afrika wajadili changamoto za wahamiaji

30 Novemba 2010

Mkutano wa ngazi ya juu wa maafisa wa serikali kutoka Djibouti, Ethiopia, Somalia na Yemen wanakutana kujadili jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na wahamiaji mchanganyiko kwenye pembe ya Afrika.

Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Djibouti unafanyika tarehe mosi na pili Desemba na pia utaangazia njia za kuimarisha ushirikiano katika mipaka baina ya nchi hizo nne kwa kubadilishana taarifa.

Kila mwaka maelfu ya watu kufanya safari hatari kutoka katika maeneo yao kupitia Somalia na Djibouti wakielekea kuvuka Ghuba ya Aden na kuingia Yemen na hatimaye nchi za Ghaba. Kundi hilo la watu linajumuisha waomba hifadhi, wahamiaji wa kawaida, wanaosafirishwa kiharamu, na watoto wasio na wazazi, na wanajumuisha wote wanaume, wanawake, wasichana na wavulana. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter