AU yataka vikosi zaidi vya AMISOM kuisaidia Somalia

30 Novemba 2010

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limejadili suala la Somalia ambapo hali ya usalama na vikosi vya kulinda amani vya muungano wa Afrika zimekuwa ajenda kuu.

Muungano wa Afrika ambao una vikosi vya jumla ya wanajeshi 8000 kutoka Uganda na Burundi kulinda amani Somalia AMISOM unataka msaada zaidi wa jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kuwezesha muungano huo na nchi wanachaka kuongeza idadi ya wanajeshi .

Nchi mbalimbali za Afrika ziliahidi kupeleka wanajeshi wake kulinda amani Somalia lakini imekuwa vigumu kutokana na sababu kadhaa zikiwemo fedha na nyenzo za kufanyia kazi. Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Somalia Balozi Augustine Mahiga anasema bila kuongeza vikosi hivyo na msaada wa kiufundi vita vya Somalia na hali ya usalama itaendeleo kuwa tete.

Ameongeza kuwa ana imani baraza la usalama litaafiki ombi la muungano wa Afrika kuhusu kuongeza vikosi.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter