Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu zaidi wahitajika Haiti kukabili kipindupindu:WHO

Wataalamu zaidi wahitajika Haiti kukabili kipindupindu:WHO

Haiti inahitaji madaktari zaidi 350 na wauguzi 2000 kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu limesema shirika la afya duniani WHO.

Pia wafanyakazi wasaidizi 2,200 na wauguzi wasaidizi 30,000 wa huduma za jamii wanahitajika. WHO inasema mfumo wa afya ya jamii wa Haiti unakabiliwa na mapungufu mengi na yamekuwepo hata kabla ya tetemeko la ardhi la Januari, na kuzuka kwa mlipuko wa kipindupindu kumefanya hali kuwa mbaya zaidi.

Fadela Chaib kutoka WHO anasema vifo hivi sasa ni zaidi ya 1600 na watu zaidi ya 72,000 wanapata matibabu kwenye hospitali mbalimbali.

(SAUTI YA FADELA CHAIB)

WHO inakadiria kwamba visa zaidi ya 400,000 vya kipindupindu huenda vikaripotiwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, lakini imeongeza kwamba hali hiyo inaweza kuepukwa endapo Wahaiti na washirika wao wa afya watachukua hatua za kuzuia na kutibu ugonjwa huo.