Upigaji kura Ivory Coast umefanyika kwa mazingira ya kidemokrasia licha ya mivutano:UM

Upigaji kura Ivory Coast umefanyika kwa mazingira ya kidemokrasia licha ya mivutano:UM

Duru ya pili ya uchaguzi wa Urais nchini Ivory Coast hapo jana imefanyika katika mazingira ya Kidemokrasia licha ya matukio ya mivutano na ghasia lizizosababisha vifo vya watu watatu.

Hayo yamesemwa leo na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Y.J.Choi katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi na kutoa wito wa kuwepo na hali ya utulivu wakati huu matokeo ya awali yakisubiriswa.

Bwana Y.J.Choi ambaye pia ni mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Ivory Coast UNOCI amesema mpango huo wa Umoja wa Mataifa umetiwa moyo kubaini kwamba waangalizi wote watano iliowaandaa kuwasilisha wagombea wote walikuwepo kwenye vituo vya kupigia kura.

Mpiganaji Rais Laurent Gbagbo amekuwa akichuana kwenye kinyang'anyiro hicho na waziri mkuu wa zamani Alassane Outtara kwenye duru ya pili baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Oktoba 31 kutotoa mshindi wa moja kwa moja.

Bwana Choi amewahahakikishia Waivory Coast kwamba wanaye mshirika wa kutegemea ambaye ni jumuiya ya kimataifa na kwamba UNOCI itaendelea kuisaidia nchi hiyo katika juhudi za kumaliza migogoro ya kisiasa.