Skip to main content

UM wakataa kutoa kauli kuhusu nyaraka zilizotolewa na Wikileaks

UM wakataa kutoa kauli kuhusu nyaraka zilizotolewa na Wikileaks

Umoja wa Mataifa umesema hautotoa tamko kuhusu nyaraka zilizochapishwa wavuti ya kufichua mambo ya Wikileaks.

Nyaraka hizo zinadai kwamba maafisa wa Marekani wanawachagiza wanadiplomasia kukusanya taarifa kuhusu maafisa wa Umoja wa Mataifa na shughuli zao.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Umoja wa Mataifa hauwezi kutoa tamko lolote kwani uhakika wa nyaraka hizo haujadhibitishwa.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice pia amekataa kutoa maelezo yoyote kuhusu nyaraka hizo lakini amewatetea wanadiplomasia wa nchi yake.

(SAUTI YA BI SUSAN RICE)