Wanajeshi zaidi ya UM watumwa nchini Ivory Coast

Wanajeshi zaidi ya UM watumwa nchini Ivory Coast

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeamuru kutumwa kwa wanajeshi zaidi wa kulinda amani wa umoja huo kwenda nchini Ivory Coast kabla ya awamu ya pili ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi huu.

Vikosi ya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Ivory Coast UNOCI vimekuwa vikikabiliana na ghasia katika mji mkuu Abijan. Umoja wa Mataifa pia umezitaka nchi za magharibi mwa Afrika kuhakikisha kuwa uchaguzi wa amani umeandaliwa nchini Ivory Coast. Aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo atawania kiti hicho pamoja aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Alassane Quattara kwenye uchaguzi unaofanyika baada ya awamu ya kwanza ya uchaguzi iliyoandaliwa mwezi Oktoba mwaka huu. Uchaguzi huo ambao ulipangwa kundaliwa mara ya kwanza mwaka 2005 umekuwa ukihairishwa tangu wakati huo.