Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali mbaya nchini Pakistan baada ya mafuriko: UNICEF

Hali mbaya nchini Pakistan baada ya mafuriko: UNICEF

Ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF uliozuru maeneo ya Shadatkot na Sindh nchini Pakistan kati ya tarehe 21 na 23 mwezi huu unasema kuwa maneo ya vijiji ya sehemu hizo yameharibiwa kabisa huku wanaorejea makiwa wakikosa nyumba , chakula , shule au njia zozote za kujikimu kimaisha kufuatia mafuriko makubwa yaliyoyakumba maeneo hayo. Hadi leo UNICEF imepokea dola milioni 169 kati ya ya dola milioni 251 ilizoomba. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF:

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Huku wengi wa wakimbizi wa ndani wakirejea kwenye mkoa wa Sindh bado maji yaliyoterema yanawazuia baadhi yao kurejea nyumbani. Shule 271 bado zinatumika kama makao zikiwa na idadi ya watu 40,000 kati wengine wengi bado wakiwa wamesalia kambini. Idara ya kitaifa inayohusika na kutoa onyo la mapema kuhusu kutokea kwa magonjwa inasema kuwa kuna uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ukiwemo ugonjwa wa surua , ugonjwa wa kuhara pamoja na ugonjwa wa pepopunda.