Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa wito wa kubadili mbinu za kusaidia nchi maskini

UM watoa wito wa kubadili mbinu za kusaidia nchi maskini

Kulingana na ripoti iliyolewa na Umoja wa Mataifa ni kuwa usaidizi wa kimataifa unaotolewa hivi sasa kwa nchi maskini zaidi, umeshindwa kuchangia kukua kwa uchumi na maendeleo ya nchi hizo na hivyo mbinu tofauti zinastahili kutumika kuziinua nchi hizo.

Ripoti hiyo iliyotolewa na mkutano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo UNCTAD inaangazia maendeleo kwenye nchi maskini zaidi na kuelezea vile jamii ya kimataifa inaweza kuzisadia nchi hizo. Cheick Sidi Diarra mwakilishi wa nchi maskini na nchi za visiwa zinazoendelea anasema kuwa usaidizi wa kimataifa kwa nchi maskini haujachangia kukua kwa nchi hizo. Ripoti hiyo inasema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kasi ya kupunguza umaskini kwenye nchi maskini ilikuwa chini hata kama kulishuhudiwa ukuaji wa uchumi.

Ripoti hiyo inaonyesha jinsi mipango ya kuzisaidia nchi maskini ilivyopiga hatua kwa muongo mmoja uliopita na kutoa uamuzi kuwa mipango ya sasa haikuzaa matunda jinsi ilivyotakiwa.