Skip to main content

UM watangaza mikakati ya kufanikisha duru ya pili ya uchaguzi nchini Ivory coast

UM watangaza mikakati ya kufanikisha duru ya pili ya uchaguzi nchini Ivory coast

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast ametangaza hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuwezesha duru ya pili ya uchaguzi ujao unafanyika katika mazingira ya uwazi na ukweli.

Nchi hiyo iliyoko Afrika magharibi inatazamiwa kuwa na duru ya pili uchaguzi wa urais hapo siku ya jumapili, kufuatia uchaguzi wa awali wa October 31.

Mjumbe huyo Y. J. Choi amesema kumeweka utaratibu ambao utahakikisha kwamba zoezi la upigaji kura, uhesabuji wa matokeo na usafirishwaji wa kura hizo hadi kwenye vituo vya majumuisho unafanyika katika hali ya uwazi na ukweli.

Kwenye upigaji kura huyo rais Laurent Gbagbo anayewania muhula mwingine anatazamia kuchuana na Waziri Mkuu wa zamani Alassane Ouattara,