UM yalaani mauwaji ya mwaandishi wa habari Iraq

24 Novemba 2010

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kuwalinda waandishi wa habari, amelaani vikali tukio la kuuliwa kwa mwandishi mmoja wa habari nchini Iraq, mauji ambayo yanafanya jumla ya waandishi wa habari waliuwawa katika kipindi cha mwaka huu kufikia 15.

Mwandishi huyo wa habari Mazen Mardan al-Baghdadi ambaye alikuwa akifanya kazi na kituo kimoja cha luninga alikutwa ameuwawa na watu wasiojulikana.

Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO imesema kuwa mwandishi huyo aliuwawa mwishoni mwa wiki nje ya nyumbani kwake katika mji wa Mosul.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter