Siku ya kimataifa kutokomezwa kwa dhuluma dhidi ya wanawake kuadhimishwa kesho tarehe 25

24 Novemba 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kuna hatua zilizopigwa kote duniani ambapo watu wanaungana kumaliza dhuluma dhidi ya wanawa na watoto wasichana.

Akiongea kabla ya maadhimisho ya siku ya kimatiafa ya kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake tarehe 25 mwezi huu Ban amesema kuwa watu wengi zaidi wanaendelea kuelewa kuwa dhuluma za kijinsia ni tatizo la kila mmoja na kuwa kila mtu ana jukumu ya kumaliza tatizo hilo. Naye mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay ametoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidhi ya uovu wanaotendewa wanawake wazee au vijana. Amesema kuwa kila siku kila mmoja kati yetu anastahili kuwa mtetezi wa haki za binadamu na kuzuia ubaguzi dhidi ya wanawake. Amesema kuwa kuwa mataifa yana jukumu la kulinga wanawake wao lakini mara nyingi hayafanyi bidii katika suala hilo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter