Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka kurejewa kwa mazungumzo mashariki ya kati

UM wataka kurejewa kwa mazungumzo mashariki ya kati

Umoja wa Mataifa umetaka kuondoshwa kiwingu kinachotatiza kuanza tena mazungumzo ya mashariki ya kati ambayo yalivunjika hivi karibuni kufuatia Israel kuendeleza na ujenzi wa makazi ya walowezi katika ukingo wa Gaza.

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja huu anayehusika na masuala ya siasa Lynn Pascoe amezitaka pande zote mbili Palestina na Israel kurejea upya kwenye meza ya majadiliano lakini akasisitiza kuwa lazima Israel isitishe mpango wake wa ujenzi.

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ametishia kutorejea kwenye majadiliano iwapo wapinzani wake wataendelea na mpango wa ujenzi wa makazi ya walowezi.