Skip to main content

MONUSCO yaanza operesheni ya kuwalinda raia na watoaji misaada ya kibinadamu

MONUSCO yaanza operesheni ya kuwalinda raia na watoaji misaada ya kibinadamu

Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vilivyopo Jamhuri ya kidemokrasia (DRC) vimetangaza kuanzisha oparesheni maalum yenye lengo la kuwalinda raia wa nchi hiyo pamoja na wafanyakazi wa kutoa misaada dhidi ya makundi ya waasi ambayo yamekuwa yakichafua hali ya hewa kwenye eneo hilo.

Vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa (MONUSCO) vimesema operesheni hiyo ambayo imepewa jina la KINGA YA NGAO itaendeshwa katika jimbo la Kivu Kusin kwenye maeneo ya Minembwe,Fizi pamoja na Uvira sehemu ambazo zimeripotiwa kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na makundi ya waasi dhidi ya wananchi wa kawaida pamoja na mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu.

Makundi hayo ya waasi pia yameshambuliana kwa risasi na jeshi la taifa. MONUSCO inaamini kuwa kukamilika kwa operesheni hiyo kutafungua milango kwa raia waliyokimbia makazi yao kurejea nyumbani.