Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu nchini Iran zinatia mashaka:Navi Pillay

Haki za binadamu nchini Iran zinatia mashaka:Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo Jumanne amerejea kuelezea hofu yake juu ya hatma ya watetezi wa haki za binadamu nchini Iran na hasa Bi Nasrin Sotoedeh ambaye amekuwa kwenye mgomo wa kula kwa wiki kadhaa kwenye gereza la Evin mjini Tehran.

Bi Pillay kesi ya bi Nasrin ni sehemu tuu ya wapigania haki za binadamu wengi walio katika matatizo na kushikiliwa nchini Iran na ni hali inayoongezeka na kutia mashaka makubwa kuhusu hatma yao. Ameongeza kuwa mashirika kadhaa pia watu wake wamekamatwa na kuhukumiwa katika miezi ya karibuni nchini humo.

Amesema uhuru wa kuongea na kukusanyika ni haki ya kisheria ya kimataifa na iko kwenye mikataba ya kimataifa ya haki za kijamii na kisiasa ambayo Iran imetia saini.