Skip to main content

Waathirika wa mafuriko Pakistan wahofia majira ya baridi:ICRC

Waathirika wa mafuriko Pakistan wahofia majira ya baridi:ICRC

Maelfu ya waathirika wa mafuriko ya Pakistan kwenye jimbo la Khyber Pakhtunhkwa wanakimbizana na wakati kabla ya kuwasili kwa majira ya baridi, hasa kujenga upya nyumba zao, kuondoa mabaki ya uharibifu wa mafuriko na kupanda mazao.

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA na kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC wanotoa msaada kwa waathirika wanasema changamoto kubwa kwa wakulima ni kulima na kupanda mazo yanayohimili baridi kabla ya kiwango cha joto kushuka sana.

Mashine za kulimia zilizogawiwa na ICRC zimekuwa zikifanya kazi usiku na mchana kuandaa mashamba na pia ICRC imewagawia wakulima mbegu na mbolea kama sehemu ya maandalizi kama anavyofafanua Chriatian Cardon wa ICRC.

(SAUTI YA CHRISTIAN CARDON)

ICRC inasema kwa Pakistan mazao hayo sio tuu ynawalisha mamilioni ya watu kwa mwaka mzima bali pia ynawaletea kipato baada ya kuuza au kubadilishana na bidhaa zingine .