Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindu bado ni changamoto kubwa Haiti:WHO

Kipindupindu bado ni changamoto kubwa Haiti:WHO

Vifo vilivyosababishwa na kipindupindu nchi Haiti vimeongezeka na kufikia 1300 huku wengine zaidi ya 23,000 wameathirika kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

WHO inasema walioambukizwa ni pamoja na watoto 5700 walio chini ya umri wa miaka mitano, na wengine 100 ni miongoni mwa waliokufa.Limeongeza kuwa pia idadi ya walioathirika huenda ikiwa bni kubwa zaidi kutokana na kwamba wengi hawawezi kupata huduma au kufika kwenye vituo vya afya na kuorodheshwa.

Shirika hilo linasema miundombinu kuwawezesha kumfikia kila muathirika bado ni changamoto kubwa lakini kila juhudi zinafanyika kuhakikisha madawa na vifaa vinafika kwenye vituo vya afua Claire Chaiignat ni mkuu wa kitengo cha kudhibiti kipindupindu cha WHO.

(SAUTI YA CLAIRE CHAIGNAT)

Nalo shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA kati ya dola 164,000 ilizoomba kukabili kipindupindu Haiti ni dola milioni 6.8 pekee zilizopatikana hadi sasa. Mkuu wa OCHA Valarie Amos aliyewasili Haiti leo anasema ni muhimu fedha hizo kupatikana .