23 Novemba 2010
Utafiti huo unasema mchanganyiko wa dawa ya kurefusha maisha ikinywewa kila siku, pamoja na matumizi ya mipira ya condom inapunguza hatari ya maambukizi kwa asilimia 43.8kwa wanaume na wanawake waliobadili jinsia zao na kujamihiana na wanaume.
UNAIDS na WHO imepongeza utafiti huo uliofanywa na jopo la watafiti wa iPrEx. Wanaume wanaoshiriki ngono na wanaume wenzao mara nyingi wanatengwa, ni vigumu kuwafikia na hawawezi kupata huduma za kuzuia virusi vya HIV. Takwimu mpya za utafiti huo zimekusanywa katika nchi 43.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WHO Margaret Chan majaribio hayo yanafungua matarajio mapya wa wanaume wanaoshiriki ngono ya jinsia moja ingawa amesema bado kuna majaribio kadhaa yatakayoendelea kufanyika. Kwa nchi karibu 80 duniani zimeharamisha ngono za jinsia moja na kwingine ni kosa la jinai.