Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhisho la vita Afghanistan ni mazungumzo:Ban

Suluhisho la vita Afghanistan ni mazungumzo:Ban

Suluhisho la vita vya Afghanistan litategemea na mazungumzo na ari ya kisiasa miongoni mwa Waafghanistan.

Hiyo ni tathimini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye ameshiriki mkutano wa NATO kuhusu Afghanistan uliofanyika mjini Lisbon Ureneo mwishoni mwa wiki. Jeshi linaloongozwa na NATO linaisaidia serikali ya Afghanistan kujenga jeshi lake la ulinzi na usalama ili liweze kukabiliana na wanamgambo wa Taliban.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba kipindi cha mpito cha kukabidhi kwa Waafghanistan hali ya kuchagiza amani na usalama wao utakuwa ni mchakato wa hatua kwa hatua.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)