Bunge la Somalia kumbatieni amani:Mahiga

Bunge la Somalia kumbatieni amani:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amelitaka bunge la mpito la nchi hiyo kulikubali baraza jipya la mawaziri kwa kile alichokiita njia ya kuelekea amani ya taifa hilo la pembe ya Afrika.

Dr Augustine Mahiga amesema watu wa Somalia na jumuiya ya kimataifa wanasubiri kwa hamu kuundwa kwa baraza la mawaziri linalofanya kazi.

Somalia haina serikali kuu tangu kupinduliwa kwa utawala wa Muhammad Siad Barre mwaka 1991.Ghasia zinazoendelea Somalia zimewalazimisha watu zaidi ya milioni mbili kuzikimbia nyumba zao na kuwa wakimbizi wa ndani na nje.