Ushirikiano wa Kusini-Kusini wakutana Geneva
Mkutano mkubwa wa kimataifa wenye lengo la kuchagiza na kubadilishana uzoevu wa suluhu ya changamoto za maendeleo zinazoikabili dunia umeenza leo mjini Geneva.
Mkutano huo ambao umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP kitengo cha ushirikiano wa kusini-kusini unafanyika kwenye makao makuu ya shirika la kazi duniani ILO. Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yan, mashirika ya hisani na yanayohusika na mipango ya maendeleo yanahudhuria mkutano huo.
Miongoni mwa wazungumzaji wakuu ni Rais wa zamani wa Chile na mkurugunzi mkuu wa chombo cha Umoja wa Mataifa cha wanawake UN-Women Bi Michelle Bachelet, waziri wa mambo ya nje wa Brazili Celso Amorin na mkurugenzi mkuu wa ILO Juan Somavia.
(SAUTI YA JUAN SOMAVIA)
Lengo kubwa la mkutano huo ni kubaini, kuchagiza na kubadilishana uzowevu wa ushahidi wa suluhu ambazo zinaweza kusaidia kuongeza kasi ya kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ikiwa imesalia miaka mitano tuu kabla ya muda wa mwisho hapo 2015.