Skip to main content

Makubaliano ya Copenhagen yanaweza kupunguza joto duniani kwa nyusi joto mbili?

Makubaliano ya Copenhagen yanaweza kupunguza joto duniani kwa nyusi joto mbili?

Huku serikali zikijiandaa kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mjini Cancun Mexico mwezi huu ripoti mpya inaonyesha kuwa ahadi zilizotolewa na serikali miezi 12 iliyopita ni ishara ya ulimwengu kupunguza kupanda kwa joto duniani .

Ripoti hiyo iliyoratibiwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP ni kati ya ushirikiano na wataafiti 30 wa masula ya hali hewa na taasisi barani Asia , Ulaya , Amerika Kusini na Marekani. Ripoti hiyo inaangazia hali mbaya zaidi na bora zaidi hadi mwaka 2020 na viwango vya gesi chafu vinavyostahili kukomeshwa ili kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti hiyo itatolewa kwa vyombo vya habari tarehe 23 mwezi huu na mkurugenzi wa UNEP Achim Steiner.