Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zatibua juhudi za kuakabiliana na kipindupindu Haiti

Ghasia zatibua juhudi za kuakabiliana na kipindupindu Haiti

Ghasia zinazoendelea kushuhudiwa kwenye sehemu mbali mbali nchini Haiti zinatatiza juhudi za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa ghasia hizo zimevuruga kupelekwa kwa madawa huku walioambukizwa hawana uwezo wa kufika kwenye vituo vua afya kupata matibabu.

Zaidi ya watu 18,300 wanapata matibabu ya ugonjwa wa kipindupindu hospitalini wakati wengine 1,110 wakiaga dunia kutokana na ugonjwa huo. UNICEF inakadiria kuwa asilimia 12 ya waliokufa ni watoto walio chini ya miaka mitano. Gregory Harlt ni kutoka shirika la WHO.

(SAUTI YA GREGORY HARTL )

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu inasema kuwa ugonjwa wa kipindupindu umesambaa hadi jela za Haiti na hadi sasa umesababisha vifo vya takriban wafungwa kumi na tano.