Ikiadhimishwa siku ya maliwato UM wahimiza usafi duniani

19 Novemba 2010

Kamati inayohusika na haki za kibinadamu hii leo inatarajiwa kuafikia makubalino ya kuyashawishi mataifa kuhakikisha kuwa kila mmoja bila ya ubaguzi ana ahaki ya kuishi katika mazingira safi.

Kamati hiyo inayohusika na masuala ya uchumi , jamii na haki za utamaduni inasema kuwa suala la usafi limesahaulika hata kama bado watu bilioni 2.6 hawaishi kwenye mazingira safi huku wengine zaidi ya bilioni moja hawana vyoo.

Kamati hiyo inasema kuwa kwenye nchi zinazoendelea asilimia 80 ya maji taka yanaingia moja kwa moja kwenye maziwa , mito na baharini na kutokana na hili magonjwa ya kuhara ndicho chanzo kikuu ya vifo vya watoto walio nchi ya miaka mitano kwenye nchi hizi.

Kamati hiyo pia imesema kuwa kutokuwepo kwa mazingira safi kumeathiri masomo hususan miongoni mwa watoto wasichana baaada ya kuabukizwa magonjwa yanayosababishwa na kukaaa kwenye mazingira chafu . Mara nyingi watoto wasichana hukosa kuhudhuria masomo katika sehemu nyingi za ulimwengu kutokana na ukosefu wa vyoo au kutotengewa vyoo vyao.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter