Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni ya watoto wakabiliwa na dhulma duniani:UM

Mamilioni ya watoto wakabiliwa na dhulma duniani:UM

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ghasia dhidhi ya watoto Marta Santos Pais anasema kuwa ghasia na dhuluma dhidi ya watoto bado vinaendelea kuwahangaisha mamilioni ya watoto kote duniani.

Santos aliyasema hayo hii leo kwenye maadhimisho ya haki za watoto kuunga mkono siku ya kimataifa iliyopendekezwa ya kupinga dhuluma na ghasia dhidi ya watoto. Flora Nducha na taarifa kamili

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Ukatili dhidi ya watoto bado unafichwa na kukubalika katika jamii , ina athari kubwa na za muda mrefu kwa maisha ya watoto zikiwemo za kimwili, kiakili na kihisia. Pia athari hizo zinagusa maendeleo yao na elimu yao amesema Santos Pais.

Ukatili wa kimapenzi unahusishwa na unyanyapaa na machungu ya moyoni na unasababisha mamba zisizotakikana, magonjwa ya zinaa na hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya HIV kwa wavulana na wasichana.

Ameongeza kuwa ingawa vitendo hivyo ni ukiukaji mkubwa wa haki za watoto lakini ubakaji, ulawiti na ukatili bado ni vigumu kuvifanyia utafiti kutokana na unyeti wake.Takwimu zilizoko ni hafifu na hazitoshelezi, huku tafiti za kitaifa ni chache na kutoa taarifa ya vitendo hivyo ni vigumu.