Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kuwalinda wahudumu wa afya kuambukizwa HIV na TB wazinduliwa

Mpango wa kuwalinda wahudumu wa afya kuambukizwa HIV na TB wazinduliwa

Mashirika ya kimataifa yakiwemo shirika la kazi duniani ILO, shirika la afya duniani WHO pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maradhi ya ukimwi UNAIDS yanazindua mpango wa kuwakinga wahudumu wa afya kutokana na kuambukizwa virusi vya ukimwi na ugonjwa kwa kifua kikuu.

Mpango huo unatarajiwa kuwafaidi karibu wahudumu milioni sitini wa afya kote duniani wanaochangia kwa njia moja au nyingine katika kazi za utoaji wa huduma za afya wakiwemo wauguzi, wakunga, wafanyikazi wa mahabara , wale wanaodumisha usafi na madaktari.

Mkurugenzi wa ILO anayehusika na usalama wa kijamii Assane Diop anasema kuwa mpango huo utahakikisha kuwa wahudumu wa afya wanapata njia za kujikinga dhidi ya maradhi ya kifua kikuu na ukimwi, na pia wanapata kutibiwa na kufidiwa ikiwa wameambukizwa na pia kupewa bima wakiwa kazini.

Wakati mashirika ya UNAIDS ,ILO na WHO yamekuwa yakiunga upatikanaji wa haki ya kupata huduma za kujikinga kuambukizwa pamoja na matibabu dhidhi ya maradhi ya ukimwi suala la kushughulikia maslahi ya wahudumu limekuwa likisahaulika.