Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matarajio ya kurudi nyumbani kwa waathirika wa mafuriko Pakistani yaendelea kusalia kwenye ndoto.

Matarajio ya kurudi nyumbani kwa waathirika wa mafuriko Pakistani yaendelea kusalia kwenye ndoto.

Mamia ya watu nchini Pakistan ambao maeneo yao yalikubwa na mafuriki makubwa bado wameendelea kukabiliwa na hali ngumu ikiwemo kushindwa kurejea majumbani mwao na kuendelea kuishi kwenye hali dunia.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) hata hivyo limeendelea na jitihada ya utoaji wa misaada ya dharura ambayo hata hivyo imezidiwa kutokana na kuzidi kuongezeka kwa mahitaji.

Wengi wameendelea kupoteza maisha na familia nyingine zimekosa makazi na chakula. Watoto wanaozaliwa kwenye hali hiyo ngumu wameshindwa kumudu mazingira na hivyo hurafiki mara kwa mara

Kutoakana na hali ngumu tayari hadi sasa UNHCR imeweka makambi yapatayo 42 ambayo yanatumika kuwahifadhia baadhi ya waathirika