SADC yataka kutelezwa kwa itifaki ya uhuru wa kusafiri

19 Novemba 2010

Mkutano juu ya suala la uhamiaji, uliowajumusha mawaziri toka eneo la Kusini mwa afrika umemalizika huko Namibia na kutoa tamko linalotaka kuwepo kwa ushirikiano wa dhati ili kushughulikia suala hilo la uhamiaji.

Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika ukiwahusisha mawaziri wanaohusika na uhamiaji katika eneo la kusini mwa afrika umetaka nchi wanachama kufanya haraka juu ya itifaki inayotaka kuondolewa kwa visingiti ili wananchi wawe na fursa ya uhuru wa kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Mkutano huo umetaka kuzingatiwa kwa itifaki iliyofikiwa katika miaka ya hivi karibuni na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa afrika SADC ambazo ziliazimia kuondoa vikwazo vya kusafiri.

Akizungumza kwenye mkutano huo Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba, alizingumzia haja ya kukabili suala la uhamiaji kwa nguvu ya umoja na wakati huo huo akataka kuondolewa kwa fikra ya kale inayotazama suala la uhamiaji katika mtizamo hasi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter