Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umeipongeza Bolivia na kusisitiza mengi yanaweza kufanywa

UM umeipongeza Bolivia na kusisitiza mengi yanaweza kufanywa

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Navi Pillay amesema kuwa licha ya serikali ya Bolivia kupiga hatua juu ya marekebisho baadhi ya sheria zake lakini hata hivyo asilimia kubwa ya watu wake wanaendelea kuishi kwenye umaskini mkubwa na kukosa fursa.

Akikamilisha ziara yake nchini humo, Kamishna huyo ambaye ziara yake hiyo ni ya kwanza kufanya amesema kuwa katiba mpya ya Bolivia inatuma ujumbe kwa mataifa mengine kuhusiana hatua ya kihistoria iliyofikiwa.

Amesema kuwa kuwepo kwa katiba inayotambua haki za msingi za kila raia na uhuru wake, ni ishara tosha inayoashiria kwamba taifa hilo limedhamiria kuheshimu misingi ya haki za binadamu. Hata hivyo ameelezea wasiwasi wake namna baadhi ya wananchi wa maeneo ya vijijini wanavyotaabika kufikiwa na haki na kushamiri kwa vitendo vya uvunjivu wa misingi inayozingatia haki za binadamu.