Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fiji yatia saini kuharamisha madawa ya kuongeza nguvu

Fiji yatia saini kuharamisha madawa ya kuongeza nguvu

Taifa la Fiji limetia sahihi makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya yanayopiga marufuku matumuzi ya madawa yanayosisimua mwili kwenye michezo na kufikisha idadi ya nchi zilizo wanachama wa makubaliano hayo kuwa 150.

Sheria za kimataifa dhidhi ya matumizi ya madawa yanayosisimua mwili yanaruhusu kufanyika kwa uchunguzi bila ya notisi kabla au baada ya mashindano zilikubaliwa na kamati ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamudni UNESCO mwezi Oktoba mwaka 2005.

Makubaliano hayo yana lengo la kuhakikisha kuwa kuna njia mwafaka za kukabiliana na matumizi ya madawa ya kusisimua misuli kwa kushurutisha serikali kuchukua hatua kuzuia kusambazwa kwa madawa hayo na ulanguzi wake.