Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ngoma na madawa ni miongoni mwa tamaduni za kale:UM

Ngoma na madawa ni miongoni mwa tamaduni za kale:UM

Tamaduni kutoka Hispania , Mexico na China ni baadhi ya tamaduni 46 zilizojumuishwa kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya tamaduni za kale.

Tamaduni hizo ziliwekwa kwenye orodha hiyo baada ya kuchaguliwa na kamati ya wanachama 24 kwenye mkutano wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO unaondaliwa mjini Nairobi Kenya.

Ili tamaduni ziweze kujumuishwa kwenye orodha hiyo ni lazima tamaduni hizo zitimize yanayohitajika yakiwemo mchango ambao zimetoa kuhusu tamaduni zenyewe na hamasisho kuhusu umuhimu wake. Orodha hiyo ya tamaduni ilizinduliwa mwezi Novemba mwaka 2008 kwa ushirikiano na shirika la UNESCO kwa lengo la kulinda kuhifadhi tamaduni za kale na hadi sasa orodha hiyo ina tamaduni 166.