Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaona juu ya dawa ya malaria kuanza kuwa sugu

WHO yaona juu ya dawa ya malaria kuanza kuwa sugu

Shirika la afya duniani WHO limesema juhudi za kupambana na malaria huenda zikapata pigo endapo usugu dhidi ya dawa ya artemisini hautoangaliwa ipasavyo.

Usugu dhidi ya dawa ya Artemisinn hivi sasa umebainika zaidi kwenye mpaka wa Cambodia na Thailand, lakini WHO inahofia kwamba huenda ukasambaa kwenye maeneo mengine duniani ikiwepo Afrika. Shirika hilo limetoa wito kwa wizara za afya kwenye nchi zinazokabiliwa na malaria kuwa makini zaidi kwa kufuatilia jinsi dawa hiyi inavyofanya kazi jambo ambalo litasaidia kubaini mapema usugu dhidi ya dawa hiyo.

(SAUTI YA MSEMAJI WA WHO)

WHO inasema malaria inauwa watu 860,000 kila mwaka, na asilimia 90 ya vifo hivyo vinatokea katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.