UM wakaribisha hatua ya Israel kuondoa vikosi Lebanon

UM wakaribisha hatua ya Israel kuondoa vikosi Lebanon

Uamuzi wa Israel wa kuondoa wanajeshi wake katika kijiji cha Ghajar kwenye mpaka kati ya Lebanon na eneo la Syria linalokaliwa na Israel, umekaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Serikali ya Israel jana Jumatano imekubali ombi la Umoja wa Mataifa la kuondoa vikosi vyake kutoka kwenye kijiji hicho na kupeleka vikosi hivyo kwenye eneo la Kusini mwa mpaka wake na Lebanon eneo linaloitwa msitari wa bluu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ban Ki-moon kujiondoa kwa Israel Kaskazini mwa Ghajar itakuwa ni hatua kubwa katika kuelekea kutekeleza azimio la baraza la usalama la kutatua mgogoro wa 2006 kati ya Israel na Lebanon.