Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafungwa wa kisiasa Myanmar waachiliwe:Ban na Suu Kyi

Wafungwa wa kisiasa Myanmar waachiliwe:Ban na Suu Kyi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwanaharakati wa kupigania demokrasia nchini Myanmar aliyeachiliwa huru mwishoni mwa wiki Daw Aung San Suu Kyi wamesisitiza haja ya serikali ya Myanmar kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa waliosalia gerezani nchini humo.

Katika mazungumzo yao kwa njia ya simu wote wameafiki kwamba inabidi waachiliwe haraka ili wananchi wote Myanmar wawe huru kuchangia katika matarajio ya maridhiano ya kitaifa, upatanisho na kipindi cha mpito cha demokrasia nchini humo.

Ban ambaye amempongeza pia Suu Kyi wa ujasiri na utu wake unaotoa hamasa kwa mamilioni ya watu duniani amemwambia mwanaharakati huyo kwamba ametia moyo na taarifa yake ya kutaka maridhiano kwa kutoa omboi la mazungumzo na muafaka baada ya kuachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani.

Ban amesisitiza kwamba ataendelea kuzichagiza pande zote Myanmar kutumia fursa hii kushirikiana kwa manufaa ya taifa kupitia majadiliano.

Suu Kyi kwa upande wake ameshukuru jukumu la Umoja wa Mataifa nchini Myanmar na kusisitiza umuhimu wa jukumu hilo na juhudi za Katibu Mkuu alizozifanya kwa niaba yake.