Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zimepigwa Afrika katika kutokomeza ukeketaji kwa wanawake:UNICEF

Hatua zimepigwa Afrika katika kutokomeza ukeketaji kwa wanawake:UNICEF

Hatua kubwa zimepigwa katika juhudi za kutokomeza ukeketaji kwa wanawake barani Afrika licha ya shinikizo la mila na utamaduni katika suala hilo.

Hayo yamo kwenye ripoti mpya ya utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Ripoti hiyo inasema ukeketaji bado unafanyika kwa kiasi kikubwa nchini Ethiopia, Misri na Sudan ,ikiongeza kwamba kukomesha mila hiyo iliyomea miziz kwa karne nyingi ni mchakato wenye changamoto kubwa na utachukua muda.

UNICEF inasema jamii ni lazima zichagizwe kuachana na ukeketaji kwa njia zisizo za vitisho zikiwa ni pamoja na kukumbatia mila bora na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inashughulikia matatizo ya jamii. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MERIXIE MERCADO)

Inakadiriwa wasichana zaidi ya milioni tatu barani Afrika wako katika hatari ya kukeketwa kila mwaka. UNICEF inasema ukeketaji ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwa wanawake na unaweza kusababisha matatizo ya muda mrefu ya kiafya ikiwemo ya wakati wa kujifungua na vifo kwa watoto wachanga.