Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya vyakula yatarajiwa kupanda mwaka 2011

Bei ya vyakula yatarajiwa kupanda mwaka 2011

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa huenda bei ya bidhaa nyingi ikapanda na kuzidi dola trilioni moja mwaka huu wa 2010 zaidi ya mwaka 2009.

Shirika hilo pia linatoa onyo kwa jamii ya kimataifa kujiandaa kwa nyakati ngumu zinazokuja iwapo uzalishaji wa vykula muhimu hautafanywa mwaka 2011. Bei ya vyakula kwa nchi maskini duniani inakisiwa kupanda kwa asilimia 11 mwaka 2010 na kwa asilimi 20 kwa nchi zilizo na kipato cha chini. Shirika la FAO linasema kuwa huku bei ya bidhaa muhimu ikiwa juu jamii ya kimataifa lazima iwe macho mwaka 2011 na kujiandaa zaidi. FAO pia linasema kuwa kulingana na utabiri wa mapema mavuno ya nafaka duniani yanatarajiwa kupungua kwa asilimia mbili badala ya kuongezeka kwa asilimia 1.2 jinsi ilivyotarajiwa mwezi Juni.