Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia nchini Haiti zavuruga huduma za kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu

Ghasia nchini Haiti zavuruga huduma za kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu

Taifa la Haiti limetoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa maandamano yenye ghasia ambayo yanatatiza juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Mratibu wa masuala yaa kibinadamu nchi humo Nigel Fisher amesema kuwa hali ya usalama katika eneo la Cap Haitien inatatiza kutolewa kwa huduma wakati ambapo visa vya maambukizi ya ugonjwa huo vikiendele kupanda.  Alice Kariuki na taarifa zaidi.

Bwana fisher ametoa wito kwa wanaohusika kwenye maandamano hayo kuyasitisha mara moja ili kutoa nafasi kwa mashirika ya kimataifa kuendesha huduma za kuokoa maisha ya walioambukizwa ugonjwa wa kipindupindu. Fisher anasema kuwa kila siku hospital hubaki bila madawa huku wagonjwa wakikaa bila kuhudumiwa. Amesema kuwa ni muhimu kwa kila mbinu kutumika kukabiliana na mlipuko huu wa kipindupindu katika eneo la Cap Haitien. Kwa sasa Umoja wa Mataifa umelazimika kufutilia mbali safari za ndege zinazosafirisha bidhaa kwenda Cap Haitien. Nalo shirika la afya duniani WHO limesitisha utoaji wa mafunzo kwa wahudumu wa afya wakati ghala la shirika la FAO nalo likiporwa na takriban tani 500 za chakula kuibiwa na ghala kuchomwa.