Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mcheza filamu Coleman ateuliwa kuwa "bingwa wa vijana" wa UM

Mcheza filamu Coleman ateuliwa kuwa "bingwa wa vijana" wa UM

Mcheza filamu raia wa Marekani Monique Coleman ambaye ni maarufu kwa kuigiza kwenye filamu ya "High School Musical" amepata uteuzi wa kwanza kabisa wa umoja wa mataifa kuwa bingwa wa vijana wa Umoja wa Mataifa ambapo anatarajiwa kutoa hamasisho kuhusu changamoto zinazowakumba vijana.

Bi Coleman alikabidhiwa barua ya uteuzi wake kwenye sherehe zilizoandaliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na naibu katibu mkuu kwenye idara ya uchumi na masuala ya jamii ya Umoja wa Mataifa Jomo Kwame Sundaram. Bi Coleman amesema kuwa atatumia wadhifa huo mpya kutoa mchango katika kutimiza malengo ya milenia yanayotarajiwa kutimizwa kabla ya mwaka 2015 akitegemea zaidi upande wa kuwainua vijana.

(SAUTI YA MONIQUE COLEMAN)

 Anasema kuwa ana matumaini ya kuwasaidia vijana kutimiza malengo ya milenia kwa kuwashauri kutoa maoni yao.