Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka wananchi wa Guinea kuyakubali matokeo ya uchaguzi

Ban awataka wananchi wa Guinea kuyakubali matokeo ya uchaguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka wananchi wa Guinea kuyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais duru ya pili ambayo yanaonyesha kuwa mwanasiasa wa upinzani, Alpha Conde, ameshinda kwa asilimia 52.5 ya kura.

Ametaka pande zizozotilia shaka matokeo hayo kumaliza tofauti zao kwa kufuata mkondo wa kisheria. Mpinzani wa Conde, waziri mkuu wa zamani, Cellou Dalein Diallo , amepata asilimia 47.5 ya kura. Watu waliojitokeza kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi huo wa duru ya pili ni asilimia 67.

Katibu Mkuu Ban ametaka jumuiya za kimataifa kuliunga mkono taifa hilo hasa kipindi hiki linapoanza safari ya enzi mpya.