Skip to main content

UNHCR yahamisha wakimbizi wa Sudan CAR

UNHCR yahamisha wakimbizi wa Sudan CAR

Usalama mdogo na mtatizo ya kiufundi yamelifanya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kuwahamisha wakimbizi takriban 3500 wa Sudan kutoka kambi ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati hadi katika eneo la usalama Kusini mwa nchi hiyo.

Watu 500 wameshahamishwa hadi sasa kwa kutumia ndege zoezi linalofanyika kwa ushirikiano wa UNHCR na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Zoezi hilo lililoanza wiki iliyopita litaendelea kwa mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa Andrej Mahecic msemaji wa UNHCR watu wengi walikimbia nchini kwao Juni 2007 kuepuka mapigano haliki hali ya usalama imezidi kuwa mbaya katika eneo hili kwa wiki mbili zilizopita na ni sababu kubwa ya kuwahamisha.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)