Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama limetoa wito wa hatua ya haraka kuchukuliwa kuhakikisha amani, uwazi na utulivu kwa kura ya maoni Sudan

Baraza la usalama limetoa wito wa hatua ya haraka kuchukuliwa kuhakikisha amani, uwazi na utulivu kwa kura ya maoni Sudan

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali ya Sudan na kusisitiza kwamba hali ya nchi hiyo ni moja ya changamoto kubwa zinazolikabili baraza la usalama.

Akiwasilisha taarifa ya Rais wa baraza hilo waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague amesema baraza la usalama linaendelea na mtazamo wa kuheshimu na kusaidia Sudan kuwa huru, yenye amani na utulivu na kuwa na mustakabali utakaozingatia matakwa ya Wasudan wote kwa kutekeleza makubaliano ya amani ya CPA yalitotiwa saini 2005 ambayo moja ya vipengele ni kuhakikisha kura ya maoni inafanyika kwa Sudan Kusini na eneo la Abyei.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwasilisha ripoti yake kuhusu Sudan kwenye baraza hilo amesema ni muhimu sana kuzingatia matakwa ya watu wa Sudan na kudumisha amani na usalama.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)