Skip to main content

Syria yahitaji kupiga hatua zaidi hata baada ya maendeleo kwenye afya UM

Syria yahitaji kupiga hatua zaidi hata baada ya maendeleo kwenye afya UM

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya kupata huduma za afya ameitaka Syria kufanya juhudi zaidi kuhakikisha kuwa wananchi wake wamepata huduma bora.

Hata baada ya kulipongeza taifa hilo la mashariki ya kati kwa kuimarisha huduma za afya Anand Grover amesema kuwa jitihada zinazofanywa ili kuboresha sekta ya afya nchini Syria ni ishara tosha. Grover pia amesema kuwa kupunguzwa kwa vifo vya watoto nchini Syria kunaisongesha Syria karibu na ulimwengu uliondelea katika masuala ya afya. Mtaalamu huyo pia ametoa wito wa kuwepo kwa hamasisho kuhusu dhuluma za kijinsia na kuhakikisha kuwa wanawake wanapata haki zao.