Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Graca Machel azuru Zimbabwe kuunga mkono haki za watoto

Graca Machel azuru Zimbabwe kuunga mkono haki za watoto

Mtetezi wa haki za watoto wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Graca Machel hii leo amewasili nchini Zimbabwe kuiunga mkono serikali ya nchi hiyo katika juhudi zake za kuimarisha haki za watoto na kuimarisha masuala ya elimu na afya.

Ziara hiyo ya bi Machel inajiri wakati Zimbabwe inaonekana kupiga hatua kwenye masuala ya kutoa huduma za kijamii kufuatia kuanza kuimarika kwa uchumi. George Njogopa na taarifa kamili:

Ziara yake hiyo ambayo imeratibiwa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na watoto UNICEF, inatilia msisitiza uwekezaji kwenye huduma za kiafya ili hatimaye kuboresha maisha na ustawi wa watoto.

Akizungumzia juu ya suala hilo Bi Grace Machel amesema kuwa itakuwa siyo jambo la busara kuacha watoto wanatapa tapa na kulipa gharama kutokana na kuanguka kwa hali ya uchumi wa Zimbabwe. Amesema kuwa kwa hivi sasa watoto wengi wanapoteza maisha kutoaka na magonjwa mbalimbali kutokana na kukosa kinga hivyo lazima sasa kuanza kutilia kipaumbele kubadilisha hali hiyo.

Ziara ya Bi Machel nchini Zimbabwe inakuja wakati ambapo nchio hiyo ikakabiliwa na changamoto kubwa juu ya ubora wa maisha ya watoto huku kukizuka magonjwa mbalimbali.