Mkutano wa nne juu ya mkataba wa matumizi ya tumbaku kufanyika Uruguay

Mkutano wa nne juu ya mkataba wa matumizi ya tumbaku kufanyika Uruguay

Mkutano wa nne wa kimataifa unaojadiliwa juu ya mkataba wa matumizi ya tumbaku unatazamiwa kufanyika huko: Punta del Este, Uruguay kuanzia Novemba 15-20.

Wajumbe zaidi ya 600 kutoka nchi zaidi ya 170 wanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo na wanatazamiwa kuibua mikakati mipya itayofanikisha utekelezaji wa mkataba huo.